NLC Yakamilisha Ushirikishwaji wa Umma Kuhusu Rasimu ya Kanuni za dhuluma za kihistoria za Ardhi (HLI) na Mapitio ya Ruzuku na Utoaji wa Ardhi ya Umma Huko Lamu

Kisiwa cha Lamu, Kaunti ya Lamu

02/10/2026

Tume ya Kitaifa ya Ardhi (NLC) siku ya Ijumaa ilikamilisha zoezi la ushirikishwaji wa umma kuhusu Rasimu ya Kanuni za Dhuluma za Kihistoria za Ardhi (HLI) na Rasimu ya Kanuni za Mapitio ya Ruzuku na Utoaji wa Ardhi ya Umma lililofanyika katika Chuo cha Anuwai cha Lamu (Lamu Polytechnic), Kisiwa cha Lamu, Kaunti ya Lamu.

Zoezi hilo liliwapa wananchi, wawakilishi wa jamii, viongozi wa serikali ya kaunti na wadau mbalimbali kutoka Kanda ya Pwani fursa ya kupitia rasimu ya kanuni hizo zinazopendekezwa, kutoa maoni na mapendekezo yao kuhusu masuala yanayohusiana na dhuluma za kihistoria za ardhi pamoja na mapitio ya ruzuku na Utoaji wa ardhi ya Umma.

Timu ya NLC iliongozwa na Kamishna Mheshimiwa Mohamed Abdi Mohamed , akiambatana na Mkurugenzi wa Masuala ya Kisheria na Utatuzi wa Migogoro, Brian Ikol Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Bwana Igalu aliwahimiza wakazi wa Lamu kuchangia kikamilifu ili kuboresha rasimu hizo na kuiwezesha Tume kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande wake, Kamishna Abdi aliwashukuru wakazi kwa kujitokeza kwa wingi na kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo. Alipokea na kutambua michango ya thamani iliyotolewa na washiriki kuhusu malengo na vipengele muhimu vya rasimu za kanuni hizo.
Ushiriki huo wa umma ni sehemu ya azma ya Tume ya kuendeleza utawala wa ardhi unaojumuisha wote, wenye uwazi na uwajibikaji. Maoni na mapendekezo yaliyokusanywa wakati wa zoezi hilo yatachangia katika kuboresha na kukamilisha kanuni hizo zinazopendekezwa.

Tume ilitoa shukrani za dhati kwa wananchi wa Kaunti ya Lamu na wadau wote kutoka Kanda ya Pwani kwa ushiriki wao na michango yao ya thamani katika mchakato huo.

Kabla ya zoezi hilo, Kamishna  Mohammed alifanya ziara ya heshima kwa Kamishna wa Kaunti ya Lamu Bwana Stephen Sangolo na Gavana wa Lamu Mheshimiwa Issa Timmamy, ambaye aliipongeza Tume kwa juhudi zake katika kuimarisha usimamizi bora wa ardhi katika eneo hilo.

error: Content is protected !!